KATIBA YA MTANDAO WA VIJANA LIWALE-(MVILI)
LIWALE YOUTH NETWORK-(LIYONE)
UTANGULIZI
DIRA YETU
DHIMA YETU
IBARA YA I
1.0: SEHEMU YA I JINA
1.2: ANAUANI NA MAHALI
1.3: ASILI
IBARA YA II
2.0: MALENGO YA MVILI/LIYONE
IBARA YA III
2.2: MAMLAKA
IBARA YA IV
3.0: UANACHAMA (MVILI/LIYONE).
3.2.0: HADHI YA MWANACHAMA
3.3.0: UKOMO WA MWANACHAMA
3.4.0: HAKI NA WAJIBU WA MWANACHAMA
IBARA YA V
4.1.0: UONGOZI WA KIKUNDI/ASASI
4.1.1:KAMATI TENDAJI
IBARA YA VI
5.0: MAJUKUMU YA VIONGOZI WA KIKUNDI/ASASI
5.1.0: MWENYEKITI MTENDAJI
5.1.1: MAKAMU MWENYEKITI MTENDAJI
5.2.0: KATIBU MKUU MTENDAJI
5.3.0: MWEKA HAZINA
6.O: MKUTANO MKUU
6.2.0: SHUGHULI ZA MKUTANO MKUU.
6.3.0: MKUTANO MKUU MAALUM
7.0: CHOMBO CHA USHAURI (UBALOZI)
8.0: MASWALA YA FEDHA
9.0: MABADILIKO YA KATIBA YA MTANDAO WA VIJANA LIWALE
9.2.0: KUVUNJWA KWA KIKUNDI.
KATIBA YA MTANDAO WA VIJANA LIWALE-(MVILI)
LIWALE YOUTH NETWORK-(LIYONE)
ASASI ISIYO YA KISERIKALI NA ISIYO YA KUPATA FAIDA
UTANGULIZI
Vijana ndiyo kundi rika kubwa katika jamii yetu ya sasa ya Liwale na hata taifa kwa ujumla.Uwepo wa wingi
huo wa vijana unatoa uhakikisho wa uwepo wa nguvu kazi na nguvu fikra za kutosha ambazo ni hitaji muhimu
sana kwa Maendeleo endelevu ya jamii yetu ya sasa na ya baadae.
Hata hivyo nguvu kazi na nguvu fikra hizo za vijana, ili ziwe na tija stahiki na tarajiwa kwa jamii ni sharti
ziendelezwe kwenye uwelekeo chanya.
̎Hakuna kesho nzuri ya Liwale kama vijana watapuuzwa - ̎ waasisi.
Hivyo kwa kuzingatia, vijana wa Liwale wamegawanyika katika makundi mbalimbali yasiyoungana na
yasiyoshirikiana kwa hiyo ni nadra kuleta tija itarajiwayo katika jamii na;
Kwa kuwa, mazingira yetu ya sasa tuliyomo yanakosekana jukwaa unganishi ambalo kama vijana
tungeweza kuchangia mawazo,fikra,changamoto,
uzoefu na kubadilishana ujuzi kwa Maendeleo yetu na Maendeleo ya jamii yetu kwa ujumla.
Hivyo basi tumeshawishika kuanzisha Mtandao wa Vijana utakaolenga kuunganisha vijana na kuziba kabisa
ombwe linalofifisha jitihada za vijana kuwa na tija stahiki kwa jamii.
DIRA YETU
Kuwa na Liwale iliyostawi yenye kizazi cha vijana wenye uelewa na uthubutu mpana wa kushiriki kwenye
shughuli mbalimbali za kiuchumi,kijamii na kiutamaduni kwa maendelo endelevu ya jamii nzima kufikia 2035.
DHIMA YETU
Kuwawezesha vijana ili waweze kuwa na njia au mbinu bora kabisa za kushiriki na kuendeleza,fikra,
mawazo,vipaji,uelewa na uthubutu kwenye masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii kwa manufaa yao
wenyewe na ya jamii kwa
ujumla.
KAULI MBIU
“Fikra mpya matumaini mapya ishi mabadiliko”
IBARA YA I
1.0: SEHEMU YA I JINA
1.1: Jina la asasi litakuwa ni;
MTANDAO WA VIJANA LIWALE ( MVILI)
1.1: (a) Bila ya kuathiri matumizi ya jina hilo,tafsiri ya kiingereza ya jina hilo yaweza kutumika sambamba, nayo
ni;
LIWALE YOUTH NETWORK (LIYONE)
1.2: ANAUANI NA MAHALI
Makao makuu ya (MVILI/LIYONE) yatakuwa wilayani Liwale kujumuisha jengo la ofisi,anuani za posta,barua
pepe na aina nyingine yeyote ya Mawasiliano.
1.3: ASILI
Ni asasi isiyo ya kiserikali na isiyo ya kupata faida na haifungamani na chama chochote cha siasa
IBARA YA II
2.0: MALENGO YA MVILI/LIYONE
2.1: Malengo ya (MVILI/LIYONE) yatakuwa ;
i. Kuunganisha vijana walio ndani na nje ya Liwale katika kuchochea
Mabadiliko kuelekeza kuyafikia maendeleo ya vijana na jamii kwa ujumla.
ii. Kuhamasisha na kujenga uelewa mpana kwa vijana kuwa wazalendo,
waadilifu na moyo wa kujitolea kwa ajili ya maendeleo na jamii kwa ujumla.
iii. Kuhamasisha na kuanzisha kampeni mbalimbali za kujenga
uelewa kama Elimu,Afya,Mazingira na masuala mengine mtambuka.
iv. Kujenga uelewa kwa jamii dhidi ya VVU na UKIMWI
v. Kuwa sauti ya vijana/kupaza sauti za vijana katika kuelezea changamoto zao mbalimbali za kimaisha.
vi. Kuhamasisha uelewa na umuhimu wa kutunza mazingira .
vii. Kuhamasisha michezo,burudani na utamaduni katika jamii yetu.
viii. Kuandaa na kuendesha semina za kujenga uelewa katika
masuala ya kisheria,biashara na ujasiriamali.
ix. Uhilimishaji wa upashanaji wa habari katika jamii.
IBARA YA III
2.2: MAMLAKA
Ili kufikia malengo yaliyowekwa kwa mujibu wa katiba hii na si vinginenvyo, kikundi/asasi kupitia kamati
tendaji yake inaweza kutekeleza yafuatayo;
i. kuajiri vibarua au wafanyakazi wa kudumu
ii. Kukodisha au kumiliki majengo
iii. Kufungua akaunti benki
iv. Kuanzisha na kuratibu semina,warsha na matukio mbalimbali ili kujenga
uelewa kwa vijana na jamii kwa ujumla
v. Kufanya kazi za mashirika,asasi na vyombo vya kiserikali kwa kubadilishana
taarifa.
vi. Kutunisha mfuko wa kikundi/asasi kwa kutumia harambee
vii. Kupanga kiwango cha ada ya uanachama na michango mingine.
viii. Kufanya chochote ambacho hakivunji katiba na sheria za nchi kwa lengo la
kutunza mali za kikundi/asasi.
IBARA YA IV
3.0: UANACHAMA (MVILI/LIYONE).
3.1.0: Uanachama wa Mtandao wa Vijana uko wazi kwa mtu yeyote atakayetimiza vigezo vifuatavyo;
i. Awe na umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.
ii. Kuwa tayari kulipa ada ya uanachama kiasi cha TSHS 5000/=na mchango kwa mwezi TSHS 2000/=
iii. Kufuata na kutii kanuni,taratibu na miongozo mbalimbali ya kikundi.
iv. Awe na akili timamu.
v. Awe na tabia njema katika jamii
vi. Awe muadilifu
vii. Awe na mtazamo chanya wa kuleta mabadiliko ya kujenga taifa .
3.1.1: Bila kuathiri masharti yaliyowekwa (3.1.0 kuanzia kifungu kidogo cha( i – vii) shirika au asasi iliyo ndani
au nje ya wilaya inaweza kuwa mwanacha iwapo malengo yake yanafanana na (MVILI/LIYONE).
3.1.2: Bila kuathiri Masharti yaliyowekwa (3.1.0) Mtu yeyote anaweza kuwa mwanachama wa kikundi bila
kujali jinsi,rangi,dini wala aina nyingine yeyote ya ubaguzi.
3.2.0: HADHI YA MWANACHAMA
3.2.1: Kila mwanachama au shirika/asasi ndani ya kikundi watakuwa na hadhi sawa na kila mmoja atakuwa na
kura moja kwenye mkutano mkuu.
3.2.2: Kila shirika/asasi au mwanchama watateua mwakilishi kushiriki kwenye mikutano ya kukundi kwa
kutaarifu jina la mwakilishi husika kwa katibu wa kikundi.
3.3.0: UKOMO WA MWANACHAMA
3.3.1: Uanachama wa mwanchama yeyote unaweza ukatenguliwa na kamati tendaji ya kikundi kwa nia njema
lakini mwanchama atakuwa na haki ya kusikilizana na kamati tendaji kabla ya uamuzi wa mwisho kufikiwa juu
ya hatma ya uanachama wake.
3.3.2: Mwanachama kwa hiari yake anaweza kujiuzuru uanachama kwa kuuharifu uongozi wa kamati tendaji
kwa maandishi.
3.3.3: Mwanachama atakaejiuzuru ama kufukuzwa kwenye kikundi hapatakuwa na urejeshaji wa aiana yeyote
ya fidia kwa nguvu au mchango uliyotolewa na
mwanachama huyo.
3.4.0: HAKI NA WAJIBU WA MWANACHAMA
i. Kuhudhuria mkutano na kufanya maamuzi kwa kupiga kura.
ii. Kulipa ada na michango mingine kama itakavyopangwa.
iii. Kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa.
iv. Kuwa mlinzi wa mali ya chama.
v. Kutetea,kusambaza taarifa mbalimbali za kikundi daima.
vi. Kuonyesha tabia njema na maadili mazuri wakati wote.
IBARA YA V
4.1.0: UONGOZI WA KIKUNDI/ASASI
4.1.1: Kikundi/asasi itaongozwa na vyombo viwili vya kimaamuzi ambavyo ni mkutano mkuu na kamati tendaji
pamoja na chombo kimoja cha ushauri kitakachojulikana kama balozi.
4.1.1:KAMATI TENDAJI
4.1.2: Kamati tendaji itaundwa na watu wasiozidi nane (8) kati yao wataingia kwenye kamati kwa kofia za vyeo
vyao nao ni Mwenyekiti mtendaji,Katibu mtendaji na Mweka hazina. Wajumbe wengine wanaosalia
watachaguliwa kwenye mkutano mkuu wa kikundi.
4.1.3: Kamati tendaji itakua inakutana angalau mara moja(1) kila mwezi.
4.1.4: Mwenyekiti mtendaji atakua muongozaji wa vikao vyote vya kamati tendaji na kolamu ya vikao vyote
vya kamati kuu tendaji itakuwa robo tatu ya idadi ya wajumbe.
4.1.5: Upigaji kura wa kwenye vikao vyote vya kamati tendaji itafanywa kwa kunyosha kidole au kura ya siri.
4.1.6: Ikitokea kura zimefungana Mwenyekiti atakua na KURA YA ZIADA.
4.2.0: Kama ikitokea mjumbe mmoja wa kamati tendaji ameenda kinyume na matakwa ya katiba hii kamati
tendaji inaweza kwa wingi wa idadi ya kura usiopungua robo tatu (3/4) inaweza kumuondoa mjumbe yeyote
wa kamati tendaji madarakani huku ikizingatiwa kwamba mtu huyo amepewa haki ya kusikilizwa kabla ya
uamuzi wa mwisho.
4.2.1: Kamati tendaji inaweza ikamteua mtu mwingine kuwa mjumbe wa kamati tendaji kuziba nafasi
iliyoachwa wazi, ikizingatiwa robo tatu (3/4) ya kura zilizopigwa zimependekeza jina moja.
IBARA YA VI
5.0: MAJUKUMU YA VIONGOZI WA KIKUNDI/ASASI
5.1.0: MWENYEKITI MTENDAJI
i. Kuilinda na kuitetea katiba ya kikundi/asasi kwa juhudi zake,maarifa yake yote na nguvu zake.
ii. Kuwa mwenyekiti wa vikao vyote vya kamati tendaji na mkutano mkuu wa kikundi/asasi
iii. Kuongoza na kusimamia kazi za kazi za kikundi kwa mifano ya kuigwa.
iv. Kuandaa na kutoa taarifa za kikundi kwenye mkutano mkuu.
v. Kuwa mweka sahihi wa nyaraka zote za kikundi pamoja na akaunti na miamala yote ya kifedha
inayofanywa na kikundi.
vi. Kuwa msemaji na mtetezi mkuu wa kikundi.
vii. Kuliwakilisha kundi kwenye mikutano,shughuli na dhifa mbalimbali ambazo kikundi kitakua
kinaalikwa.
5.1.1: MAKAMU MWENYEKITI MTENDAJI
i. Kumsaidia Mwenyekiti mtendaji na kusimamia shuguli na majukumu kama yalivyoelekezwa kwa
mujibibu wa katiba(ibara ya v kifungu cha 5.1.0 kifungu kidogo i – vii) endapo Mwenyekti mtendaji
hayupo.
ii. Kutekeleza majukumu mengine kama yatakavyopangwa na Kamati tendaji.
5.2.0: KATIBU MKUU MTENDAJI
i. Kuitisha vikao vyote halali vya kikundi/asasi kwa kushirikiana na Mwenyekiti mtendaji.
ii. Kuwa katibu wa vikao vyote halali vya kikundi/asasi.
iii. Kupanga,kuendeleza na kusimamia shughuli za kila siku za kikundi/asasi .
iv. Kuandika na kutunza kumbukumbu,mihutasari mbalimbali ya vikao na mikutano ya kikundi/asasi .
v. Kukusanya na kusambaza taarifa mbalimbali ndani ya kikundi.
vi. Kutunza na kusimamia mali zote halali za kikundi/asasi.
vii. Kufanya shughuli zingine zozote ambazo ni halali na zitalinda maslahi ya kikundi/asasi kama
itakavyopaswa au kuamuliwa na kamati tendaji.
5.3.0: MWEKA HAZINA
i. Kubuni mbinu za kongeza mapato ya kikundi/asasi.
ii. Kuandaa,kutoa na kuweka kumbukumbu sahihi ya taarifa ya mapato na matumizi ya kikundi/asasi.
iii. Kutunza nyaraka zote halali za mahesabu za kikundi/asasi .
iv. Kupokea michango na ada za uanachama wa kikundi.
v. Kufanya malipo yote halali ya kikundi/asasi .
vi. Kuwa mweka sahihi wa nyaraka zote za kikundi pamoja na akaunti na miamala yote ya kifedha
inayofanywa na kikundi.
vii. Kufanya shughuli au majukumu yote halali ya kifedha kama yatakavyoelekezwa au kuamuliwa na
kamati tendaji.
6.O: MKUTANO MKUU
6.1.0: Kutakuwa na mkutano mkuu ambao utafanyika mwezi wa 12 kila mwaka, tarehe ya mkutano itapangwa
na kamati tendaji.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu ni Wanachama wote halali na hai wa kikundi/asasi lakini pia kuna uwezekano wa
kuwepo na wageni waalikwa kama kamati tendaji itaridhia kuwaalika.
6.1.1: Wanachama wote watapewa taarifa juu ya uwepo wa mkutano mkuu angalau siku 14 kabla ya
kufanyika kwa mkutano mkuu.
6.1.2: Akidi ya mkutano mkuu itakuwa angalau nusu(1/2) ya Wanachama wote.
6.2.0: SHUGHULI ZA MKUTANO MKUU.
i. Kupokea na kujadili taarifa ya Mwenyekiti mtendaji kuhusu shughuli za kikundi kwa mwaka nzima.
ii. Kupokea na kujadili taarifa ya mapato na matumizi ya kikundi/asasi.
iii. Kuchagua kamati tendaji ya kikundi/asasi.
iv. Kujadili jambo lolote kadili litakavyoweza kuamuliwa.
v. Kutoa mapendekezo ya kubadili katiba au kutengeza kanuni za kikundi pale inapobidi.
vi. Kuchukuwa hatua za kinidhamu dhidi ya viongozi wa kikundi/asasi waliokiuka katiba hii.
vii. Kupitisha kanuni na miongozo ya kinidhamu dhidi ya uvunjifu wa katiba, kanuni na miongozo ya
kikundi/asasi
6.3.0: MKUTANO MKUU MAALUM
6.3.1: Muda wowote kunaweza kuitishwa mkutano mkuu maalumna kamati tendaji ya kikundi/asasi
au robo ya wanachama kwa kuiharifu kamati tendaji ya kikundi kujadili jambo la dharula ,katibua
atawajulisha wanachama angalau siku 14 kabla ya kufanyika kwa mkutano mkuu maalum pamoja na
ajenda itakayojadiliwa.
7.0: CHOMBO CHA USHAURI (UBALOZI)
Kamati tendaji itaunda chombo cha ushauri kitakachojulikana kama balozi.
7.1.0: Kutakuwa na balozi shawishi na balozi unganishi.
7.1.1: Balozi shawishi itaundwa na wajumbe wazee wasiozidi watatu(3) na kazi yao kubwa nikutoa
ushauri mbalimbali kwenye mipango na shughuli za kikundi.
7.1.2: Balozi unganishi nazo zitaundwa na wajumbe vijana si zaidi ya watatu na kazi yao kubwa
itakuwa kuunganisha vijana kwenye maeneo watayowepo
7.1.3: balozi shawishi na balozi unganishi ndio zitakuwa ndio balozi zetu nje ya makao makuu yetu au
nje ya wilaya.
8.0: MASWALA YA FEDHA
i. 9.0: Pesa yeyote itakayokusanywa na balozi itatumika kwa malengo ya kikundi.
ii. Akaunti ya benki itakayofunguliwa itakuwa na jina la kikundi.
iii. Malipo au miamala yeyote halali lazima lazima iandikwe na kumbukumbu zake zitunzwe.
iv. Watia sahihi katika akaunti ya kikundi lazima wawepo jumla wajumbe au wanachama
wasiopungua watano (5).
9.0: MABADILIKO YA KATIBA YA MTANDAO WA VIJANA LIWALE
9.1.0: Katiba inaweza kubadilishwa yote au kifungu kimoja kama zaidi ya theluthi mbili (2/3) ya wanachama
watakubali mapendekezo hayo na kuyapigia kura ya ndiyo kwenye mkutano mkuu.
9.2.0: KUVUNJWA KWA KIKUNDI.
9.2.1: Kikundi kinaweza kuvunjwa kama zaidi ya theluthi mbili (2/3) ya wanachama wataunga mkono maamuzi
hayo kwenye mkutano mkuu.
9.2.2: Kama kikundi kitavunjwa baada ya madeni kulipwa kama yapo,
Mali na Pesa za kikundi zinaweza kuhamishiwa katika kikundi kingine ambacho kina malengo yanayofanana
au ikitokea hakutokuwepo kwa kikundi/asasi namna hiyo, Mali na Pesa hizo zitatolewa kwenye familia ama
watu masikini wasiojiweza.
NAMBA YA SIMU 0787700088
EMAIL: 2015mvili@gmail.com
0 comments:
Post a Comment