Sunday, January 3, 2016

                                   MTANDAO WA VIJANA LIWALE-(MVILI)
                                       LIWALE YOUTH NETWORK-(LIYONE)
                        ASASI ISIYO YA KISERIKALI NA ISIYO YA KUPATA FAIDA
                                                           
                                                        UTANGULIZI
Vijana ndiyo kundi rika kubwa katika jamii yetu ya sasa ya Liwale na hata taifa kwa ujumla.Uwepo wa wingi
huo wa vijana unatoa uhakikisho wa uwepo wa nguvu kazi na nguvu fikra za kutosha ambazo ni hitaji muhimu
sana kwa Maendeleo endelevu ya jamii yetu ya sasa na ya baadae.
Hata hivyo nguvu kazi na nguvu fikra hizo za vijana, ili ziwe na tija stahiki na tarajiwa kwa jamii ni sharti
ziendelezwe kwenye uwelekeo chanya.
̎Hakuna kesho nzuri ya Liwale kama vijana watapuuzwa - ̎ waasisi.
Hivyo kwa kuzingatia, vijana wa Liwale wamegawanyika katika makundi mbalimbali yasiyoungana na
yasiyoshirikiana kwa hiyo ni nadra kuleta tija itarajiwayo katika jamii na;
Kwa kuwa, mazingira yetu ya sasa tuliyomo yanakosekana jukwaa unganishi ambalo kama vijana
tungeweza kuchangia mawazo,fikra,changamoto,
uzoefu na kubadilishana ujuzi kwa Maendeleo yetu na Maendeleo ya jamii yetu kwa ujumla.
Hivyo basi tumeshawishika kuanzisha Mtandao wa Vijana utakaolenga kuunganisha vijana na kuziba kabisa
ombwe linalofifisha jitihada za vijana kuwa na tija stahiki kwa jamii.
                                                    DIRA YETU
Kuwa na Liwale iliyostawi yenye kizazi cha vijana wenye uelewa na uthubutu mpana wa kushiriki kwenye
shughuli mbalimbali za kiuchumi,kijamii na kiutamaduni kwa maendelo endelevu ya jamii nzima kufikia 2035.
                                                 DHIMA YETU
Kuwawezesha vijana ili waweze kuwa na njia au mbinu bora kabisa za kushiriki na kuendeleza,fikra,
mawazo,vipaji,uelewa na uthubutu kwenye masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii kwa manufaa yao
wenyewe na ya jamii kwa
ujumla.
                                                KAULI MBIU
                         “Fikra mpya matumaini mapya ishi mabadiliko”

                           2.0: MALENGO YA MVILI/LIYONE
2.1: Malengo ya (MVILI/LIYONE) yatakuwa ;
i. Kuunganisha vijana walio ndani na nje ya Liwale katika kuchochea
Mabadiliko kuelekeza kuyafikia maendeleo ya vijana na jamii kwa ujumla.
ii. Kuhamasisha na kujenga uelewa mpana kwa vijana kuwa wazalendo,
waadilifu na moyo wa kujitolea kwa ajili ya maendeleo na jamii kwa ujumla.
iii. Kuhamasisha na kuanzisha kampeni mbalimbali za kujenga
uelewa kama Elimu,Afya,Mazingira na masuala mengine mtambuka.
iv. Kujenga uelewa kwa jamii dhidi ya VVU na UKIMWI
v. Kuwa sauti ya vijana/kupaza sauti za vijana katika kuelezea changamoto zao mbalimbali za kimaisha.
vi. Kuhamasisha uelewa na umuhimu wa kutunza mazingira .
vii. Kuhamasisha michezo,burudani na utamaduni katika jamii yetu.
viii. Kuandaa na kuendesha semina za kujenga uelewa katika
masuala ya kisheria,biashara na ujasiriamali.
ix. Uhilimishaji wa upashanaji wa habari katika jamii.

                                          2.2: MAMLAKA
Ili kufikia malengo yaliyowekwa kwa mujibu wa katiba hii na si vinginenvyo, kikundi/asasi kupitia kamati
tendaji yake inaweza kutekeleza yafuatayo;
i. kuajiri vibarua au wafanyakazi wa kudumu
ii. Kukodisha au kumiliki majengo
iii. Kufungua akaunti benki
iv. Kuanzisha na kuratibu semina,warsha na matukio mbalimbali ili kujenga
uelewa kwa vijana na jamii kwa ujumla
v. Kufanya kazi za mashirika,asasi na vyombo vya kiserikali kwa kubadilishana
taarifa.
vi. Kutunisha mfuko wa kikundi/asasi kwa kutumia harambee
vii. Kupanga kiwango cha ada ya uanachama na michango mingine.
viii. Kufanya chochote ambacho hakivunji katiba na sheria za nchi kwa lengo la
kutunza mali za kikundi/asasi.

 

                                       3.0: UANACHAMA (MVILI/LIYONE).
3.1.0: Uanachama wa Mtandao wa Vijana uko wazi kwa mtu yeyote atakayetimiza vigezo vifuatavyo;
i. Awe na umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.
ii. Kuwa tayari kulipa ada ya uanachama kiasi cha TSHS 5000/=na mchango kwa mwezi TSHS 2000/=
iii. Kufuata na kutii kanuni,taratibu na miongozo mbalimbali ya kikundi.
iv. Awe na akili timamu.
v. Awe na tabia njema katika jamii
vi. Awe muadilifu
vii. Awe na mtazamo chanya wa kuleta mabadiliko ya kujenga taifa .
3.1.1: Bila kuathiri masharti yaliyowekwa (3.1.0 kuanzia kifungu kidogo cha( i – vii) shirika au asasi iliyo ndani
au nje ya wilaya inaweza kuwa mwanacha iwapo malengo yake yanafanana na (MVILI/LIYONE).
3.1.2: Bila kuathiri Masharti yaliyowekwa (3.1.0) Mtu yeyote anaweza kuwa mwanachama wa kikundi bila
kujali jinsi,rangi,dini wala aina nyingine yeyote ya ubaguzi.
 

                                        3.2.0: HADHI YA MWANACHAMA
3.2.1: Kila mwanachama au shirika/asasi ndani ya kikundi watakuwa na hadhi sawa na kila mmoja atakuwa na
kura moja kwenye mkutano mkuu.
3.2.2: Kila shirika/asasi au mwanchama watateua mwakilishi kushiriki kwenye mikutano ya kukundi kwa
kutaarifu jina la mwakilishi husika kwa katibu wa kikundi.
 

                                   3.3.0: UKOMO WA MWANACHAMA
3.3.1: Uanachama wa mwanchama yeyote unaweza ukatenguliwa na kamati tendaji ya kikundi kwa nia njema
lakini mwanchama atakuwa na haki ya kusikilizana na kamati tendaji kabla ya uamuzi wa mwisho kufikiwa juu
ya hatma ya uanachama wake.
3.3.2: Mwanachama kwa hiari yake anaweza kujiuzuru uanachama kwa kuuharifu uongozi wa kamati tendaji
kwa maandishi.
3.3.3: Mwanachama atakaejiuzuru ama kufukuzwa kwenye kikundi hapatakuwa na urejeshaji wa aiana yeyote
ya fidia kwa nguvu au mchango uliyotolewa na
mwanachama huyo.
                        

                                3.4.0: HAKI NA WAJIBU WA MWANACHAMA
i. Kuhudhuria mkutano na kufanya maamuzi kwa kupiga kura.
ii. Kulipa ada na michango mingine kama itakavyopangwa.
iii. Kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa.
iv. Kuwa mlinzi wa mali ya chama.
v. Kutetea,kusambaza taarifa mbalimbali za kikundi daima.
vi. Kuonyesha tabia njema na maadili mazuri wakati wote.
Next
Newer Post
Previous
This is the last post.

0 comments:

Post a Comment