mechi kati ya Vijuso Fc Vs Wakaanga Sumu mchezo uliochwa katika uwanja wa shule ya msingi Muungano Liwale Mjini hii leo
Leo
ikiwa May 4 katika Ligi ya Mbuzi vijana Cup inayoendelea hapa wilayani
Liwale siku ya leo kulikuwa na mchezo wa aina yake katu ya VIJUSO Vs
WAKAANGA SUMU mchezo uliotimua vumbi katika uwanja wa shule ya msingi
Muungano.
Katika
kipindi cha kwanza cha mchezo timu ya Vijuso ilikuwa ya kwanza
kujipatia goli lililofungwa katika dakika 29 kupitia mchazaji wao Yuba
Mmocha na dakika ya 38 wakaanga sumu waliweza kusawazisha goli na mapaka
mapumziko walikuwa wamefungana moja kwa moja.
Kipindi
cha pili kilianza kila timu walicheza mcheo mkali zaidi na wa kasi
lakini timu ya Vijuso ilizidiwa na kasi hiyo ndivyo wapizani wao
waliweza kutumia nafasi hiyo na kuweza kuongoza magoli 3,magoli ya
Wakaanga sumu yaliyofungwa katika dakika 53,dakiaka 65 na la tatu na la
mwisho lilifungwa na Muba katika dakika 83 na mpaka mpira unamalizika 90
matokeo yalikuwa Vijuso 1-4 Wakaanga Sumu.
Kesho May 5 kutakuwa na mchezo kati ya timu ya Kigamboni Vs Nangando mchezo utakaochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Muungano Liwale Mjini.
0 comments:
Post a Comment